Na Bakari Madjeshi,Globu ya jamii

UMOJA wa Wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani (DIHK) umewasili nchini Tanzania kwa lengo la kufungua ofisi jijini Dar es Salaam yenye kazi maalum yakuratibu wawekezaji kutoka nchini kwao.

Umoja huo chini ya Mtendaji Mkuu wake, umeambatana na wafanyabiashara na Jumuiya ndogo ya wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani na Mjumbe wa Kamati ya Bunge la Ujerumani (Anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara).

Akizungumza leo Dar es Salaam baada ya mazungumzo na Umoja huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Godffrey Mwambe amesema umoja huo umekuja nchi kufahamu mazingira ya biashara.Pia kuonesha dhamira yakuwekeza pamoja na kufanya biashara na Tanzania ambapo 

Mwambe amesema awamu hiyo ya pili ya ziara kwa Wajerumani kutua nchini ni sababu yakuwepo kwa hali ya Utulivu, ukuaji wa uchumi na mazingira mazuri ya kiutawala katika Serikali iliyopo chini ya Rais John Magufuli anayepambana na rushwa na kuondoa urasimu ndani ya Serikali yake.

“Mpaka sasa Wajerumani wana miradi 157 hapa nchini iliyosajiliwa na TIC, kwa hiyo wakija kwa wingi katika maeneo yetu na hasa kupitia mpango wetu wa miaka mitano wa maendeleo, na wakiingia kwenye viwanda tuna uhakika tutapata teknolojia ya hali ya juu na ajira kwa vijana wengi wa Kitanzania.

"Pia kujifunza teknolojia ya Kijerumani yenye sifa kubwa barani Ulaya”, amesema Mwambe na kutoa mwito kwa wafanyabishara na wajasiriamali kuhakikisha wanatumia fursa ya ujio na kuimarika kiuchumi.Ameongeza mara nyingi wawekezaji wanapokuja nchini huwa wanataka kampuni za ndani kwa lengo la kushirikiana nazo.

Pia ameziomba taasisi za Serikali kurekebisha mifumo ya utoaji huduma kwa kuhakikisha zinakuwa nzuri kwa wale wanaokuja nchini kuwekeza.Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa umoja huo, Dk.Martin Wansleben amesema wamekuja nchini kutokana na Bara la Ulaya na Afrika ni majirani na kufafanua Ulaya inahusika katka maendeleo ya chi za Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...