RS TABORA

SERIKALI imezitaka jamii kujiunga na mifuko ya huduma za bima za jamii ili waweze kupata huduma ya tiba kwa gharama nafuu badala ya kutumia mtindo wa kulipa fedha taslimu wanapokwenda kutibiwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Nzega na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wakazi wa Zogolo mara baada ya kukizindua.

Alisema kazi wananchi ambapo hajajiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii(CHF) na mingine wanajikuta wakitumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu wakati wangekata Bima za viwango tofauti wangenufaika.

Waziri huyo alisema mtu akimkatia mtoto wake mdogo Bima ya Afya ya shilingi elfu 50 atapata huduma za matibabu mwaka mzima katika Hospitali yoyote hapa nchini zikiwemo za binafsi ambazo zina makataba na Serikali kupitia Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa. Aliwataka Madereva wa boda boda wilayani Nzega nao kujiunga na Bima kwa kulipia shilingi 76000 ili waweze kupata matatibu mwaka mzima popte pindi wanapopata ajali au wanapougua na kuongeza kuwa kwa kutegemea fedha taslimu ni gharama kubwa.

Waziri huyo aliwambia wakijunga pamoja na kutoa kiasi hicho atawaunganisha ili waweze kupata vitambulisho vya Bima ambavyo vitawaweze kupata matibabu kwa gharama nafuu na fedha nyingine kuzielekeza katika shughuli nyingine za maendeleo. “unapokwenda kufanyiwa upasuaji unaweza kutozwa shilingi 100,000/- lakini ukiwa umetoa shilingi elfu 30 kupitia kujiunga Mfuko wa Afya ya Jamii , utatumia kadi kupata huduma hiyo katika Hospitali yoyote bila kudaiwa chochote” alisisitiza Ummy

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri alisema kuwa mwitikio wa wananchi Mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) bado uko chini na kuongeza kuwa wameamua kuendesha elimu kupitia mikutano mbalimbali kwa lengo la kuongeza idadi inaongezeka.

Alisema kuwa sehemu kubwa ya wakazi ni wakulima ambao wanategemea mavuno ya msimu kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ikiwemo matibabu na hivyo kupata shida wakati mwingine kwa kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama kwa fedha tasilimu kwa kuwa fedha zinakuwa hazipo tena hadi mavuno mengine.

Mwanri alisema njia ya pekee ya kuwasaidia wakulima ni kuhakikisha wengi wao wamejiunga na Mfuko wa Jamii ambapo wakitoa shilingi 10,000 wanapata matibabu watu sita katika familia moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...