Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Yusra Ali Ramadhani (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 83 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imewazawadia wateja wake 84 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

‘Katika promosheni hii murwa, Tigo inatoa bure jumla ya simu janja 12 kila siku. Pamoja na haya, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter,’

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo, ambapo kufikia sasa tumewazawadia wateja 756 simu hizi janja zenye uwezo wa 4G’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.

Kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Hamisi Mohammed Yusuph (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...