Utekelezaji
wa mazao ya kimkakati hasa Pamba msimu wa 2017/2018 kama ilivyoelekezwa
na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim watekelezwa kwa vitendo wilayani
Gairo.
Hayo
yameelekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven
alipotembelea Wilaya ya Gairo mwanzoni mwa wili iliyopita ili
kuhamasisha kilimo cha Pamba ambapo ekari moja ya pamba unapata shilingi
milioni 1.4. Alidha Dkt. Kebwe alirudi wilayani Gairo kukagua
utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo kutembelea mashamba darasa ya
viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe, Mwenyekiti wa
Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes
Mkandya.
Mhe.
Mchembe alimpa taarifa Mkuu wa Mkoa kuhusu kilimo cha pamba ambapo
hekta 181 zimelimwa, pembejeo zimepokelewa ikiwemo mbegu za pamba kilo
3,996 viuadudu mililita 120 na mabomba 10. Mbali na Pamba wilaya ya
Gairo wameweza kulima zao la Korosho ekari 2,618 jumla ya miche 70,800
pamoja na zao la kahawa idadi ya miche 800 na mbegu gramu 3,000.
Pamba,
Korosho na Kahawa ni mazao ya kimkakati na ya kibiashara hapa wilayani
Gairo ambapo mazao hayo yatawainua na wananchi kutoka uchumi wa chini
kwenda uchumi wa kati kama ambavyo sera za awamu ya tano za Rais Dkt.
John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza. Mwisho wananchi wa Gairo
walimshukuru sana Mkuu wa Mkoa, Dkt. Kebwe Steven kwa kazi kubwa
anayofanya kuhamasisha Kilimo cha mazao ya kimkakati Wilaya ya Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua shamba darasa la Mhe. Mchembe Mkuu wa Wilaya Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akiongea na wananchi Kijiji cha Kisitwi Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua kiwanda cha mvinyo itokanayo na ndizi. Kiwanda hicho ni kati ya viwanda vipya 6 vilivyoanzishwa mwaka 2018.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo Mhe. Rahel Nyangasi akiwa kwenye shamba darasa lake la zao la Pamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...