Ni kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa Wataalamu mbalimbali walioudhuria kongamano la The East Africa (EA) Innovation Event la kampuni mama ya TBL Group ya ABInBev lenye lengo la kuleta mapinduzi ya kilimo kupitia sayansi na teknolojia lililoandaliwa na taasisi ya Bits&Bites Technology Convention na kufanyika jijini Dar es Salaam, wamedhihirisha kuwa mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini na barani Afrika kwa ujumla yanawezekana kupitia matumizi ya teknolojia za kisayansi. 

 Kongamano hilo ambalo lilijumuisha wataalamu wa fani ya kilimo,watafiti,wahandisi na wabunifu kutoka kanda ya Afrika Mashariki walijadili jinsi ya kupata ufumbuzi wa kuinua kilimo cha wakulima wadogo kupitia teknolojia za kisasa na za gharama nafuu ambapo pia walishiriki shindano la ubunifu wa nyenzo za kiteknolojia ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kazi zao walizogundua.

 Makampuni ya Imara Tech,Mobisol na Back Save Equipment yaliibuka na ushindi baada ya jopo la majaji waliokuwa wanasimamia shindano hilo kubainisha kuwa ugunduzi wao wa nyenzo za kiteknolojia unaweza kusaidia kuinua maisha ya wakulima wadogo.Kazi zilizowapatia ushindi washiriki zitaanza kufanyiwa majaribio kabla ya mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa ambao ni wakulima hususani wadogowadogo.

 Akiongea wakati wa kufunga kongamano hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Sembeye, alisema kuwa kongamano hili limefanyika kwa wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga kuingia katika uchumi wa viwanda ambao unaenda sambamba na kufanya mapinduzi ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda vitakavyoanzishwa,pia kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha.

 Sembeye, alisema njia pekee ya kuleta mapinduzi ya kilimo ni kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa na za gharama nafuu ambazo wakulima wengi wa hali ya chini wanaweza kumudu kuzinunua na kuzitumia kwa ajili ya kuwawezesha kupata tija na ufanisi katika kazi zao. 
Washindi wa shindano la ubunifu wa kiteknolojia katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...