NA TIGANYA VINCENT
HATIMAYE wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) mkoani Tabora kwa kauli moja wameridhia kuganishwa kwa Chama Kikuu cha Ushirika kwa ajili ya kuchukua Wilaya za Urambo na Kaliua ili kuanzisha chama kingine kipya cha maeneo hayo.

Hatua hiyo imefikiwa na viongozi kutoka Vyama vya Msingi (AMCOS)mbalimbali kwenye Mkutano Mkuu wa 25 ulifanyika jana mjini Tabora.

Kaimu Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule alisema uamuzi wa kuchukua baadhi ya wanachama wa WETCU na kuanzisha Chama kipya ni kurahisisha usimamizi wa vyama vya msingi na kutekeleza agizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuvunja Bodi ya WETCU kwa sababu ya kushindwa  kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alisema kuwa WETCU itaendelea kubaki na usajili wake wa awali na itakuwa na Vyama vya Msingi(AMCOS) kutoka Uyui, Tabora Manispaa, Nzega na Sikonge.

Haule aliongeza kuwa kisheria kama Chama cha WETCU kingevunja ingechukua hata miaka miwili kuanzisha kingine na baada ya kufanyika ufilisi na ndipo chama kipya kianzishe , ndio maana wameona ni vema kiendelee na usajili ule ule na kianzishwe kipya kitakacho hudumia Urambo na Kaliua.

Alisema kuhusu madeni yatabaki  Chama cha  WETCU na kile kipya cha kitakachoanzishwa kitaanza bila deni kama takwa la kisheria linavyohitaji ili kiwe na sifa ya kusajiliwa.

Haule alisema viongozi wanaweza kukutana na kupendekeza jina la Chama kipya au kinaweza kuitwa UKACU ili kuendelea na taratibu za usajili na kuahidi kutangaza Bodi ya Mpito wa Chama kipya tarajiwa hivi karibuni ili hatimaye ifikapo tarehe 16 Mwezi ujao(Juni) kiwe kimesajiliwa.
 Kaimu Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule aakitoa ufafanuzi ya taratibu za ugawaji wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) na kuanzisha Chama kipya kwa ajili Wilaya za Urambo na Kaliua jana mjini Tabora wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa chama hicho.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Nathalis Linuma alitoa maoni yake jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Tumbuku Hassan Wakasubi alitoa maoni yake jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
 Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Msingi (AMCOS) wakifuatilia mada mbalimbali jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...