Na Agness Francis,  Blogu ya Jamii.
Kwa mujibu wa ofisi ya  Takwimu  ya Taifa (NBS) inaonyesha kuwa mwaka huu mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Aprili umepungua hadi kufikia asilimia 3.8 kulinganisha na mwezi Machi ambayo ilikuwa ni asilimia 3.9 .

Taasii hiyo  ya Umma ilioyoanzishwa mwaka 2015 inayosimamia na kuratibu upatikanaji wa takwimu rasmi nchini  na mfumuko wa bei  kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu  inayopima kiwango cha kasi ya mabadikiko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya  binafsi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao  Jijini  Dar es Salaam mkurugenzi wa sense ya watu na takwimu za jamii  Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungua kwa   mfumuko wa bei  kwa  mwaka  ulioisha mwezi Aprili,  mwaka huu kumechangia sana kupungua bei bidhaa za vyakula .

Kwesigabo amesema kuwa baadhi ya bidhaa za  vyakula zilizochangia mfumuko wa bei kati ya Aprili 2017 na April 2018 ni mahindi  asilimia 5.2,Unga wa mahindi asilimia 5.6,mtama asilimia 7.3,Unga wa mihogo asilimia 9.3,maharage asilimia 9.2 pamoja na mihogo mibichi kwa asilimia 13.2.

Aidha amesema kuwa hali ya mfumuko kwa Baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki hazijaachana sana kwa kulinganisha na ya taifa letu mwezi  machi na April mwaka huu.

;Kwa nchi hizi za ukanda wa Afrika mashariki Uganda umepungua  hadi asilimia 1.8 kutoka 2.0 ikiwa Kenya umepungua  hadi  asilimia 3.73 na  ilikuwa ni asilimia 4.18 kutoka mwezi machi hadi sasa Aprili mwaka huu ikiwa Tanzania ni asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.9. amesema kwesigabo.
Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 3.9 mwezi Machi hadi 38 mwezi Aprili mwaka huu, leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...