Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, leo ameshiriki  katika Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia .

Balozi Dau alishiriki kwenye mjadala huo (panellist) kwa kutoa historia ya zao la nazi Tanzania ikiwemo uzalishaji na changamoto zake. Mkutano huo wa siku 2 umeanza leo na unashirikisha Wadau wote wa zao la nazi nchini Indonesia. 

Indonesia inaongoza katika uzalishaji wa nazi Duniani kwa kulima hekta 3.6 milioni na kuzalisha nazi zaidi ya tani 17 milioni. Kwa upande wake, Tanzania inaongoza kwa zao hilo Barani Afrika lakini inalima hekta 350,000. 

Zao la nazi kwa sasa linaongoza kwa bei kwenye soko la Dunia na kulipita zao la chikichi na hata mafuta ya Petroli . Nchini Indonesia mnazi mmoja unatoa kati ya nazi 100 hadi 150 ingawa wastani wa kitaifa Ni nazi 70 kwa mnazi mmoja. 

Katika mkutano huo Balozi Dau alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Kilimo wa Indonesia Mhe Dr Amran Sulaiman ambapo walikubaliana kukuza zaidi ushirikiano kwenye kilimo baina ya nchi hizi mbili. 

Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao  kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano nk. 

Jumatatu Balozi Dau atakutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .
Pichani Balozi Dau akisisitiza jambo katika kongamano hilo 
 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...