Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia, Bela Bird leo amefungua warsha ya siku mbili kwa watalaamu na Watumishi wa Serikali kutoka nchi ya Tanzania na Malawi hili waweze kuendana mpango kazi wa Masuala ya Mazingira na Masuala ya kijamii pindi wanapotekeleza miradi inayotekelezwa na benki hiyo katika nchi hizo mbili.
Bi Bela amesema kuwa Warsha hiyo ambayo itaweza kuwasaidia watumishi wa serikali kujua miradi inayofanywa na benki ya Dunia awezi kuathiri mfumo wa Mazingira wala wanadamu wanaoishi katika eneo husika kwa namna moja ama nyingine hili kuweza kuleta usawa wa ikolojia.
"tumezunguka kama benki kwenye nchi kma 63 na kuwaeleza watu jinsi mpango kazi wa mazingira ulivyobadirika ambao una viwangoi kumi kwa kutizama masuala ya ustawi wa jamii pamoja na kutoathiri Mazingirakwa viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai."
alimaliza kwa kusema kuwa mpango kazi huo utaweza kuwasaidia watumishi wa serikali wanaosimamia miradi ya maendeleo inafadhiliwa na benki hiyo inafanikiw abila kuathiri uharibifu wa Mazingira.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somali,Bela Bird akizungumza wakati w aufunguzi wakati wa kufungua warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii Jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Benki ya Dunia, Nathale Munzberg akizungumza wakati akitoa mada wakati wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...