MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki katika kukagua miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuiepusha kujengwa chini ya kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.
Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.
Alisema iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. “Ndugu zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndio jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali kuweka utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na wakandarasi”Alisema.Nay kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia kuwatatulia mambo mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya la Makao Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amiri Sheiza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...