Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania(NIC) Sam Kamanga akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe,Hamis Dikupatile baada ya mbunge wa viti maalum mkoani Pwani ,Zainab Vullu kupokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi huyo.

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe

SHIRIKA la Bima la Taifa la Tanzania (NIC) ,limetoa msaada wa mifuko ya saruji 160 ,yenye thamani ya zaidi ya sh.mil.mbili ,wilayani Kisarawe Mkoani Pwani. Msaada huo umelenga kusaidia kumalizia miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya umma ikiwemo zahanati ,vituo vya afya na mashule katika kata zilizopo wilayani humo .

Akikabidhi msaada huo kwa mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani Zainab Vullu ,mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania, Sam Kamanga ,alisema shirika hilo linatoa misaada ya aina hiyo kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye changamoto za kijamii. Alieleza msaada huo ni moja ya kati ya shughuli za shirika za kurudisha kwa jamii.

"Katika mpango kazi wetu tumejiwekea kuwa na wananchi katika changamoto zao,Hii ni miongozo ya utawala bora kwa kuwa karibu na jamii ,tunatekeleza, tumeenza mkoani Iringa  ,Mwanza ,Sumbawanga katika sekta ya afya na elimu " alieleza Kamanga.
Mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani ,Zainab Vullu akiongea na baadhi ya madiwani na watendaji halmashauri ya Kisarawe.

Akipokea msaada huo ,mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab alishukuru shirika hilo na kusema aliongea nao juu ya ombi hilo na anashukuru amesaidia. Alisema mifuko hiyo ya saruji inaelekezwa katika kata zinazoendelea na ujenzi wa miradi ya elimu na afya.

Zainab alitaja kata hizo kuwa ni pamoja na Msimbu mifuko 20, Mafizi mifuko 30, Vihingo mifuko 30 ,Chole mifuko 10,Marumbo 10,Kazimzumbwi 10, Kiluvya 10 ,Vikumburu 10 ,Msanga 10 na kata ya Masaki mifuko kumi .

"Ndondo si chululu ,hiki tulichokipata kwangu ni kikubwa ,nawashukuru NIC kwani itakwenda kuboresha ujenzi wa mashule ,vituo vya afya na zahanati" alieleza Zainab. Mbunge huyo viti maalum Mkoani hapo ,alisema kuwa ,adhama ya serikali ni kuinua uchumi wa Viwanda na Viwanda bila waajiriwa wenye afya njema sio jambo jema .
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Bima la Taifa la Tanzania,(NIC) Sam Kamanga, akizungumza jambo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Zainab alisema madarasa yakikamilika pia huku wanafunzi wakiwa na afya njema,kwa hakika inapendeza ,alisisitiza". Aliwataka madiwani kutumia saruji hiyo kwa matumizi lengwa badala ya kuiacha bila kutumia kwa wakati na matokeo yake ije kuharibika. Zainab aliliomba shirika hilo kuendelea kuwasaidia hasa kwenye upande wa vikundi vya wanawake na vijana ili viweze kujiinua kiuchumi .

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe ,Hamis Dikupatile alisema kwasasa wilaya ipo katika mkakati wa kuondoa 0 mashuleni hivyo aliwaomba wadau na shirika hilo kuangalia namna ya kuwezesha sekta ya elimu ili kuondokana na kushuka kitaaluma .

Dikupatile alimshukuru mbunge Vullu na NIC kwa jitihada zao na kuwaomba wasichoke kuitupia macho wilaya hiyo. Alisema wilaya ya Kisarawe inaendelea kupigania maendeleo na kuinuka kiuchumi kwa maslahi ya jamii na kuondokana na umaskini .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...