Na Chalila Kibuda,Blogu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amewapongeza kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma wa Watanzania ila amehimiza pia waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, kanuni na taratibu.


Mjema ametoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa vyombo hivyo katika maendeleo ya nchi yetu.

Maadhimisho hayo yamefanywa na Jukwaa la Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukutana na kujadili masuala ya mbalimbali yanayoikumba tasnia ya habari.Kwa kukumbusha tu maadhmisho hayo duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 2 na 3 ya kila mwaka.

Mjema amehimiza pia waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, kanuni na taratibu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Waandishi wa habari Jane Mihanji amesema wanahabari wanaomba kulindwa ili watekeleze majukumu yao kwa uhuru zaidi.
Aidha changamoto ambazo zimeelezwa ikiwemo ya kukosa uhuru wa kufanya kazi ni vema nayo ikapatiwa ufumbuzi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...