Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Karagwe.
WAZAZI na walezi Mkoani
Kagera katika kuelekea msimu wa sikukuu wametakiwa kuhakikisha
wanawapatia watoto wao zawadi ya kuwaingiza kwenye mpango wa Toto afya
kadi ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.
Mkuu
wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka aliyasema hayo wakati wa uzinduzi
wa zoezi la utoaji wa Kadi za toto afya pamoja na upimaji wa afya bure
kwa wananchi wa magonjwa yasiyoambukiza zoezi lililofanyika katika stand
ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
Mheruka alisema kuwa
mzazi au mlezi kumpatia mtoto zawadi ya kadi ya toto afya ni muhimu
badala ya kumpatia zawadi ya nguo ambazo atazivaa na zitaisha."Ndugu
zangu wazazi wenzangu baada ya kumaliza kipindi hiki cha mfungo wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani zawadi nzuri ya kuwapatia watoto wetu ni
kuwaingiza katika mpango huu wa toto afya kadi kwani utamuwezesha mtoto
kuwa na uhakika wa matibabu anapougua kwa kipindi cha mwaka
mmoja"alisema Mkuu wa Wilaya
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa wataendelea kuhimiza wananchi waweze kuingiza watoto wao katika mpango huo.Meneja
wa Mfuko wa bima ya Taifa ya afya(NHIF)Elias Odhiambo alisema kuwa wiki
hii NHIF wanafanya zoezi la upimaji wa afya wananchi bure na kutoa toto
afya kadi katika maeneo ya Omurushaka na Kayanga Wilayani Karagwe.
Alisema kuwa magonjwa wanayopima wananchi ni uwiano wa uzito na refu(BMI)Kisukari,shinikizo la damu(BP)pamoja na kutoa ushauri.Odhiambo
amewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe kutumia fursa hiyo kujua hali
za afya zao sambamba na kupata elimu ya kujikinga na maradhi lakini pia
kujiunga na mfuko huo."Nawaomba wananchi wote wafike maeneo
ambayo tumeweka vituo kwaajili ya tutoa huduma ili waweze kupata huduma
kwani huduma hizi tunatoa bure"alisema
Alisema huduma ya toto
afya kadi inahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 8,ambapoatatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa
mzazi au mlezi.Alisema mwanachama wa toto afya kadi atapata
huduma zote ambazo mwanachama wa NHIF ambazo anapata na ambazo
zimeorodheshwa katika huduma.Baadhi ya wananchi waliofika katika
uzinduzi huo wameupongeza mfuko wa bima ya afya kwa jitihada zake za
kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
"Mfuko huu
umetusaidia kutuletea hii huduma ya upimaji wa afya kwani inatusaidia
kujua afya zetu lakini pia tunapata fursa ya kuujua vizuri mfuko na
huduma zake ambazo ndo mkombozi wa maisha ya kila mwananchi,tunaomba
huduma kama hizi ziwe endelevu"alisema Edson Kamugisha.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambona wananchi(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza na utoaji wa toto afya kadi katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka akimkabithi kadi ya toto afya kadi mmoja wa watoto waliopatiwa kadi katika zoezi la uzinduzi wa kupima afya bure na utoaji wa toto afya kadi kwenye stand ya magari ya omurushaka Wilayani Karagwe

Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya Taifa Mkoa wa Kagera Adam Kanza akiongea na wananchi katika stand ya magari ya Omurushaka juu ya umuhimu wa kuwakatia watoto wao toto afya kadi
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...