Na Emmanuel Masaka, Globu ya jamii.

Edith Max amemuomba Makonda kusaidia ili haki ipatikane na kufafanua nyumba yao imeporwa na moja ya taasisi na kisha kuiuza katika moja ya benki iliyopo nchini(jina tunalo).

Akieleza mkasa huo amedai familia yao ilikopa fedha Sh.milioni 30 katika benki hiyo na kudai walipotaka kulipa deni hilo walizungushwa na baadaye wakaambiwa kuna riba imeongezeka kutoka Sh.milioni 30, hadi Sh.million 90.

Amesema walikubali kulipa lakini kila wakifuatilia kulipa tena wakaendelea kuzungushwa hadi deni likafikia Sh.milioni 120 lakini walikubali kulipa fedha hiyo.Walipoenda kulipa wakabaini kuna udanganyifu umefanyika kwa kugushiwa hati ya mirathi na mtu asiyetambulika na familia.

Amefafanua familia fungua mirathi yake Januari 17 katika Mahakama ya mwanzo Kinondoni na Msimamizi wa mirathi hiyo Max Edmund Kafipa .Awali anasema, suala hili walilipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Makonda wakati wa kampeni yake ya kuwasikiliza walidhurumiwa nyumba, viwanja na mashamba iliyofanyika Januari ambapo tarehe 30 pande zote ziliitwa na kujadiliana mbele ya wanasheria na uamuzi yao yanatarajiwa kutolewa Mei 7 mwaka huu.

Hata hivyo amesema kabla ya kuanza kuvunja nyumba hiyo wahusika walipewa uzio la kutovunja lakini nyumba hiyo ikavunjwa jambo ambalo ni kinyume na sheria."Wakili wao alitamka wazi kwa Makonda hana Mamlaka ya kuingilia mambo haya na hii nyumba tulikuwa tunaitaka muda mrefu,"amesema.

Ameongeza "jana walituita wa kasema wanataka watulipe fedha.Wakatuuliza mnataka tuwape bei gani ? tukasema tulipeni Sh.bilion 2, waomba wajadiliane lakini cha kushangaza wamekuka kuvunja nyumba yetu."Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mfaume AbdulKarim Gulam Shambe amekiri kuwepo kwa sakata hilo na kwamba wakati wanakwenda kuvunja nyumba hiyo walitoa taarifa wakati wameshaanza kuivunja.

  Msemaji wa familia hiyo Edith Max (kulia)akuonesha  nyumba hiyo  jana jijini Dar as Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...