Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo Na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga Aballah Ulega amekagua mradi wa Umeme vijijini(REA) Awamu ya 3 Union delta katika Vijiji viwil vya Mkokozi na Lugwadu katika Kata ya Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumzia mradi huo leo, Ulega amesema mradi huo ua umeme unatokana na uhudi za viongozi akiwemo Diwani  wa kata aa Mwandege Adolf Kohelo na yeye Mbunge wa jimbo la Mkuranga.

 Aidha Ulega Amewashukuru  wananchi wa vijiji hivyo kwa ushirikiano wao katika kufanikisha mradi huo."Nashukuru kwa kupokea  mradi na nimesikia kuna timu ya watu wa REA wapatao 60 ambao  mmewapa ushirikiano kwa kukubali kukakata miti yenu bila gharama.Mmenitia  moyo sana," amesema.

Pia amewaomba Watanzania kumuombea Rais Dk. John  Magufuli ili andelee kuwa na nguvu ya kuwatumikia wananchi wanyonge."Wanamkuranga hakuna zawadi nzuri ya kumpa Rais zaidi ya kumuombea," amesisitiza Ulega.

Kazi ya kusimika nguzo za umeme katika vijiji vya Lugwadu na Mkokozi ikiendelea kwa kasi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na Mbunge wa Mkuranga akiwaaga wananchi wa vijiji vya Mkokozi na Lugwadu katika ziara ya kukagua mradi wa umeme wa Rea Mkoani Pwani. Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akimsikiliza Diwani wa Kata ya Mwandege,Adolf Kohelo katika ziara yake ya kukagua mrad wa umeme wa Rea Mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...