Mashindano
maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa
kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa
ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya
hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na
uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya
wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia
kuwavutia mashabiki wengi wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote
wa mbio hizo.
Katika
kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’
ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na
moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya
watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo
uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo.
Baada ya majadiliano ya kina
na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua
kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary
Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The
Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za
mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni
la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya
hisani.
Tofauti
na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye
mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya
miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam,
Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa
manufaa ya jamii.
|
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.
Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...