Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa leo ameanza kazi rasmi baada ya kukabidhiwa ofisi tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi uliopita. Bi. Agnes Mtawa anachukua nafasi ya Bi. Lena Mfalila aliyemaliza muda wake.
Awali Bi. Mtawa alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimteua kuwa Msajili wa Baraza la Uuguzi Tanzania.
Uteuzi huo ulianza rasmi tarehe 16-04-2018 na kwamba utadumu kwa muda wa miaka mitano kuanzia tarehe ya uteuzi.
Nafasi mbalimbali alizowahi kushika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Mtawa ni; Mkuu wa Mafunzo na Uajiri kuanzia mwaka 2004 hadi 2006, Mkuu wa Mafunzo, Utafiti na Elimu kuanzia mwaka 1997 hadi 2004, amewahi kuwa  Katibu Mkuu katika baraza la uuguzi na ukunga Tanzania kuanzia 2002  hadi 2011 na mwaka 2007 aliteuliwa Mkuurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi mwezi uliopita alipoteuliwa.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa leo ofisini na watumishi wa baraza hilo, huku  Bi. Jane Mazigo aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo akimpatia maua. Kulia ni Happy Masenga anayeshughulika na mafunzo katika baraza hilo.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa  akitazama zawadi ya maua aliyokabidhiwa na watumishi wa baraza hilo leo.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa kwa shangwe leo ofisini na watumishi wa baraza hilo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...