Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika akizungumza wakati akifungua mkutano wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3 waadishi wa Habari mkoa wa Mbeya wamadhimisha siku hiyo leo, Kutoka kulia ni Frank Leonard Mwenyekiti wa Press Club Iringa, Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club. KAULI MBIU ya maadhimisho hayo mkoa wa Mbeya ni "Uhuru wa Vyombo vya habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa Maendeleo ya Mkoa wa Mbeya"
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Frank Leonard Mwenyekiti wa Iringa Press Club wakati akizungumza katika mkutano huo kama mmoja wa wageni waalikwa, katikati ni Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Bi. Julieth Godrey Manech akichangia na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa upande wa Taaisis ya Kuzuia rushwa nchini TAKUKURU jinsi waandishiwa wanavyoweza kushirikiana na tasisi hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...