Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akifurahia jambo na Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na aliyewahi kuwa Msemaji wa Timu ya Yanga Bw. Jerry Muro wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikagua wachezaji wa timu ya Mashabiki wa Yanga muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya mashabiki wa Yanga na timu ya mashabiki wa Simba leo mjini Pangani.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mashabiki wa Simba muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kushoto kwake ni Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishin wa Habari muda mfupi kabala ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso ambaye ni mdhamini wa mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokea fedha taslimu shilingi milioni moja kutoka kwa Bw. Romanus Mkonda Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama mchango kwa ajili ya mashindano ya Aweso Cup.Kulia kwake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah wakishuhudia tukio hilo leo mjini Pangani.
PICHA ZOTE NA:OCTAVIAN Kimario
WHUSM


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...