Michuano ya Kurugenzi Cup 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga
imeendelea kutimua vumbi kwa timu ya Airport SC kuifunga Makulusa FC
mabao 3-0.
Katika mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi
Haydom, hadi mapumziko timu ya Airport SC ilikuwa inaongoza kwa bao
1-0 lililofungwa na Abubakary Maina dakika ya nne kwa njia ya penati.
Kipindi cha pili timu ya Airport SC ilipata mabao mawili yaliyofungwa
na mshambuliaji hatari Emmanuel Mallo kwenye dakika ya 50 na ya 55.
Kwenye mchezo mwingine timu ya Stand United timu ya Mlimani FC
iliifunga bao 1-0 na kuiondoa kwenye michuano hiyo.
Fainali ya mashindano hayo iliyoshirikisha timu 10 inatarajiwa
kufanyika jumapili ya wiki hii kwenye viwanja hivyo vya Haydom.
Katibu wa chama cha soka wilaya ya Mbulu (MBFA) Joseph Nicodemus
alisema michuano hiyo itakuwa chachu kwa vipaji vipya vya wilaya hiyo
kupiga hatua kwenye mchezo huo.
Nicodemus alisema anatarajia timu zitakazoshiriki michuano ya ligi
daraja la tatu ngazi ya wilaya zitapata wachezaji kwenye michuano hiyo
ya Kurugenzi Cup 2018.
Waamuzi wa mashindano ya Kurugenzi CUP 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga wakishuhudia manahodha wa timu ya Makulusa FC Regi Gisimoy (kulia) na Samwel wa timu ya Airport FC wakitakiana heri ya mchezo ambapo walifungwa mabao 3-0.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Airport FC wakiwa benchi la ufundi huku wakiendelea furahi mchezo ambapo waliifungwa Makulusa Fc mabao 3-0.
Baadhi ya wachezaji wakiushuhudia mpambano wa soka ukiwa unaendelea kwa kasi baina ya timu za Airtport FC dhidi ya Makulusa FC hazipo pichani.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Mmoja wa wachezaji akigangwa na madaktari baada ya kuumia mguu katika mchezo huo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...