Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
OFISA Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Evans Emil (53) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mali ambazo alijaza mshtakiwa Jenifa Mushi kwenye fomu za rasirimali na madeni ni za familia ambapo amedai mali nyingi zilizojazwa kwenye fomu hizo, zina umiliki wa nusu kwa nusu mshtakiwa na mkewe na watoto wao.
Evans ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili, Aisa Msaidizi wa Forodha Wa (TRA), Jennifer Mushi ya kukutwa akimiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake,
Akitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Shaidi huyo alidai, yeye aliajiliwa TRA mwaka 1996 akiwa na majukumu ya kushughulikia ajira, kusimamia nidhamu, maslahi ya wafanyakazi, utawala na majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
Alidai taratibu moja wapo kwa mtu ambaye atakuwa ameajiriwa na kuthibitishwa pamoja na mambo mengine anatakiwa kujaza fomu ya tamko ya rasilimari na madeni ambazo anatakiwa kuijaza kila mwaka wa kalenda na isizidi ndani ya miezi mitatu.
Alidai, fomu hizo ujazwa chini ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kanuni ya utumishi ya TRA pale mtumishi anapoajiriwa na kuripoti kazini.
Amedai, lengo kubwa la kujaza fomu hiyo ni kujua mali na madeni ya mfanyakazi na kufahamu uadilifu wa mtumishi, kutokana na mazingira ya kazi ya TRA ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa na kujilimbikizia mali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...