Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

VIJANA waliopitia Mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga taifa (JKT) wametakiwa kurejea vijijini na Kushirikiana na Halmashauri kuanzisha miradi mbalimbali na kuhakikisha wanawaelimisha vijana wengine kuondokana na umasikini kwa kutumia mafunzo waliyoyapata wakati wa kozi hiyo.

Mwito huo umetolewa na  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Brigedia Jenerali Marco Gaguti wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wakati akifunga mafunzo ya awali kwa vijana 798 wa oparesheni Mererani waliohitimu mafunzo yao ya awali katika Kambi ya Mtabila.
Ambapo aliwataka vijana hao kuondokana na mawazo ya vijana wasomi ya kutaka kuajiriwa na kuyatumia mafunzo waliyoyapata kuanzisha miradi mbali mbali na kujiajiri na kuwaelimisha vijana walioko mtaani.

Jenerali Gaguti amewataka vijana wote waliohitimu mafunzo ya oparesheni Magufuli na oparasheni  zingine kurudi katika Wilaya ya Kasulu na Buhigwe kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa kutumia mafunzo waliyoyapata na kushirikiana na vijana walioko mtaani kuhakikisha fedha zinazotolewa na Halmashauri  kwaajili ya mfuko wa vijana kutumika kuondoa umasikini .

"Nitoe mwito kupitia hadhara hii kwa vijana wote ambao ni wa Buhigwe na Kasulu na wilaya nyingine za Mkoa wa Kigoma  mrudi vijijini washirikiane na Vijana wengine waliopo mtaani, sifurahishwi na vijana wanao lalamika kuwa hakuna ajira lazima mshirikiane kuhakikisha  tunaondokana na kundi kubwa la vijana wanaodai hakuna ajira", amesema Jenerali  Gaguti.

Aidha Mkuu huyo amesema kuhusu suala la kukosekana umeme katika Kambi hiyo kulicheleweshwa na migogoro iliyokuwepo baina ya wakandarasi wa Wakala wa Umeme Vijijini( REA) awamu ya tatu ambapo mgogoro huo umemalizika na June mwaka huu wataanza kusambaza umeme wa REA  kwa Wilaya ya Kasulu na kuahidi  kuanza kuweka nguzo ya kwanza katika eneo la kambi hiyo.

Akimkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Kambi ya Mtabila  Meja   Peter Lyanga amesema wanafunzi walioanza mafunzo ya awali ya oparesheni  Mererani walikuwa wanafunzi 806 na waliohitimu ni vijana 798 na vijana nane wameshindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ugonjwa na utoro.
Amesema mafunzo waliyoyapata vijana hao yamewajenga kuwa wazarendo na kujitegemea pindi wawapo uraiani na kuwaomba vijana hao kuendelea kuyaishi mafunzo waliyojifunza  na kuhakikisha kiapo chao lakini pia wawe vijana bora kule  ndani JKT katika kipindi cha miezi 18 ya mafunzo ya stadi, kwa wale ambao hawata pata nafasi ya ajira wasikate tamaa kwani jkt limewapa stadi za maisha kutosheleza kujiari na kuongoza wengine. Mwisho amewatakia wawe tayari kulilinda taifa letu punde wakihitajika.

Wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wahitimu hao Rosemery Lyimo amesema mafanikio waliyoyapata ni kuwa na ukaka mavu na kwakujifunza kuwa na umoja bila kujali udini na ukabila pamoja na shughuli za uzalishaji mali  ambapo wameanza  kufanya kazi  pamoja na kujenga nyumba ya Mkuu wa kikosi hicho.

Amesema pamoja na Mafanikio hayo changamoto zilizojitokeza ni ukosefu wa umeme katika Kikosi na  kikosi kina uhitaji wa mwanga katika kuimarisha ulinzi na usalama, muingiliano wa Barabara baina ya kambi na wanakijiji na kuomba Changamoto hizo zitatuliwe ilikuweza kuiweka kambi salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...