SERIKALI ya Mtaa ya Upanga Mashariki Dar es Salaam imesema vitendo vya uhalifu katika mtaa huo kwa sasa vimepungua baada kuanzishwa ulinzi shirikishi wa bodadoda wa mtaa huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Rukiya Ritani amesema hayo leo kuwa wameanzisha Polisi jamii kwa kuwashirikisha madereva wa bodaboda ambao wanafanya kazi zao kwa umakini na hatimaye wamefanikiwa kupunguza uhalifu.
"Iwapo atapatikana mhalifu huwa wanamchukua na kumpeleka kituo cha Polisi ili sheria ichukue mkondo wake,"amesema Rukiya .
Amesema kwa sasa mafanikio makubwa ambayo yamepatikana wananchi wanaishi bila hofu yoyote na hata wanapopita barabarani usalama na mali zao ni mkubwa.Pia amesema mtaa huo una wakazi 4, 800 na changamoto iliyopo wanaolipa fedha kwa ajili ya ulinzi ni wachache , hivyo amewaomba wananchi kulipa fedha wa wakati.
Kwa upande wa Kiongozi wa Ulinzi shirikishi Upanga Mashariki, Seleman Abdallah amesema uhalifu umepungua kwa asilimia 85.
Mwenyekiti wa Upanga Mashariki Rukiya Ritani, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuelezea mafanikio katika ulinzi Shirikishi (Kushoto) kiongozi wa ulinzi wa mtaa huo Abdalah Seleman .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...