Na Hamza Temba - Dodoma

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa kubwa iliyopo hapa nchini ya ufugaji nyuki na uwepo wa masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao yake na kuyaongezea thamani ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo leo mbele ya wadau wa sekta ya ufugaji nyuki kutoka mikoa yote nchini katika mkutano aliouitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Amesema kwa sasa mchango wa sekta ya nyuki katika pato la taifa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo za ufugaji nyuki hapa nchini ambazo zikitumiwa ipasavyo zitasaidia kuinua pato la wananchi na taifa kwa ujumla.

Amesema mbali na kuongeza uzalishaji, mazao hayo pia yanatakiwa kuongezewa thamani na kuwekewa ngazi za ubora ili yaweze kuhimili masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, ili kuimarisha sekta hiyo Serikali itashirikiana na wadau kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kutafuta masoko, kuimarisha uwekezaji na kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta ambayo ina soko kubwa nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo. Kushoto ni MKuu wa Kitengo cha Masoko, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mwanahamisi Mapolu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Deosdedit Bwoyo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deosdedit Bwoyo akiwasilisha hotuba yake kwa wadau hao.Mkurugenzi Msaidi wa Uendelezaji Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Allen Richard akitambulisha meza kuu katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...