Na Mwandishi wetu
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amewataka vijana wa Tanzania kuwa washiriki katika mipango ya maendeleo na sio kusubiri kufanyiwa.
Aidha ameshauri vijana kuacha kuilalamikia serikali na jumuiya ya kimataifa kuhusu ajira na badala yake wajiulize wamelifanyia nini taifa na jumuiya hiyo.
Alisema katika kipindi ambacho theluthi mbili ya watu nchini ni vijana, wasitarajie kuajiriwa au kupatiwa kazi kirahisi kwa kuwa idadi ni kubwa kuliko hata yeye alipokuwa akisoma.
Alisema tatizo la ajira kwa sasa haliwezi kusubiri serikali au wahisani ni tatizo linalokuwa kibinafsi zaidi na kuhitaji vijana katika uwingi wao kuamka na kubuni vitu vitakavyoleta maendeleo yao binafsi na pia ya kitaifa.
Akizungumza katika jukwaa la vijana la AIESEC mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es salaam Mratibu huyo alisema kwamba  vijana  wanatakiwa kushiriki katika kila kitu na kuacha kushutumu serikali au jumuiya ya kimataifa katika kipindi ambacho dunia imebarikiwa na vijana  kama nguvu kazi yake kubwa.
Aliwataka vijana kujadili kuhusu malengo ya dunia, fursa zake, utekelezaji wake na changamoto zake.
“Malengo ya Dunia ni ajenga muhimu sana kwa Tanzania, Afrika na ulimwenguni  kote. Ajenda hii imelenga kuleta mabadiliko chanya kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika utekelezaji wake” alisema Alvaro na kuongeza kuwa malengo hayo 17 ni lazima yajulikane ili kil kijana ashiriki katika utekelezaji wake.
 Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo akizungumza kuhusu AIESEC na kazi zake ambapo alisema jukwaa hilo lengo lake ni kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana wa kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki kwenye jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Msimamizi wa mazungumzo ambaye pia ni Mkuu wa Mafunzo na Miradi wa Empower Ltd, Ella Naiman (kushoto) akizungumza na kuwatambulisha wazungumzaji wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd. Kutoka kulia ni Allen Kimambo, Miranda Naiman, Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga pamoja na Petrider Paul.
 Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga (katikati) akizungumza kwenye jukwaa la vijana la AIESEC  ambapo alisema vijana wanatakiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo utekelezaji wake unaishia mwaka 2030 wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mzungumzaji katika jukwaa la vijana la AIESEC, Mkurugenzi Mtendaji wa Empower Ltd, Miranda Naiman (wa pili kulia) akizungumza wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...