Na Ripota Wetu,Mbeya

Serikali imeendelea kuwasisitiza waajiri wote nchini kuwapeleka watumishi wao Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kupigwa ‘msasa’ namna ya kufanya kazi za utumishi wa umma. 

Akizungumza jijini hapa mwishoni wa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika alisema kuwa ni muhimu waajiri hao wakawapeleka watumishi chuoni hapa hasa ikitiliwa maanani kwamba TPSC ndiyo chuo kilichopewa dhamana ya kuendesha mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiri wapya wa serikali.

Alisema pamoja na makujuku hayo pia Chuo hicho kina wajibu wa kusimamia mitihani ya utumishi wa umma katika program ya kuendeleza watumishi.Pia TPSC inatoa mafunzo ya kozi nyingine za muda mrefu na mfupi katika maeneo ya uongozi, Utawala na ya matumizi ya mifumo ya kisasa ya TEHAMA.

Waziri Mkuchika aliwaasa wahitimu kwamba mafunzo waliyoyapata chuoni hapo yasiishie kwenye vyeti bali yawe ni mafunzo ya kufanya kazi kwa weledi na kasi mpya yenye ufanisi wa ili kuleta tija kwa lengo kukuza uchumi wa taifa hili.

“Ninawasihi huu usiwe mwisho wa kujiendeleza kwani mafunzo huongeza ujuzi , weledi na mbinu maridhawa za ufanisi wa kazi hususan katika kujifunza teknolojia mpya,” alisema.
Waziri wa nchi- Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Msaafu) George Mkuchika akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa Mahafali ya 28 ya TPSC chuoni hapo Jijini Mbeya. 
Mtendaji Mkuu wa TPSC Dkt Henry Mambo akizungumza wakati wa Mahafali hayo ya 28 ya TPSC Jijini Mbeya 
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 28 ya TPSC wakiwa kwenye mahafali hayo chuoni hapo Jijini Mbeya 
Baadhi ya wafanyakazi wa TPSC wakifatilia mahafali hayo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...