Wataalamu 16 toka Halmashauri za Wilaya ya Morogoro, Mvomero, Bahi, Kongwa, Kilolo na Mufindi walio chini ya Idara ya Ardhi, maliasili na mazingira wamejengewa uwezo juu ya utumiaji wa mfumo mpya na rahisi wa upimaji ardhi unaofahamika kwa jina la MAST (Mobile Application for secure tenure).

Akiongea Mkoani Iringa wakati wa ufunguzi wa ziara hiyo ya mafunzo iliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania, Donati Senzia Mratibu wa PELUM alisema lengo hasa la ziara hiyo ni kuwapatia elimu wataalamu hao na kuona ni jinsi gani wataweza kuutumia mfumo huo kwenye Halmashauri zao kupitia miradi ya upimaji ardhi ambayo watakuwa nayo. 

Akifafanua jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Mustapha Issa ambaye ni Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, alisema kuwa mfumo huu ulitengenezwa kwa ajili ya uhakiki wa maslahi na upimaji wa vipande vya ardhi ambao hutumia simu za kisasa. 

Alisema mbali na kuwa mfumo huu kutoa ajira kwa vijana wengi kama wapimaji wasaidizi baada ya kupatiwa mafunzo jinsi ya kuutumia lakini pia mfumo huu ni rahisi na hautumii muda mwingi kuanzia kwenye zoezi la upimaji, uchukuaji taarifa, utunzaji taarifa hadi kufikia hatua ya kutoa hatimiliki. 

Halikadhalika mchoro unajichora wenyewe moja kwa moja wakati wa upimaji kipande, upigaji wa picha hufanyika na kuhifadhiwa kwenye mfumo mara tu baada ya mpimaji kujiridhisha na taarifa ya mteja wake na wakati huohuo taariza zote za mmiliki wa kipande husika zinachukuliwa na kuhifadhiwa na mfumo kwa ajili ya kukamilisha zoezi la utoaji wa hatimiliki. 
Mustapha Issa  Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, akielezea jinsi mfumo wa MAST unaotumia simu za kisasa  unavyofanya kazi wakati wa upimaji wa vipande vya ardhi.
   Sadoth Kyaruzi Afisa Mpango miji na vijiji halmashauri ya Mvomero, Morogoro akichangia jambo wakati wa mafunzo ya MAST.
 Timu ya wataalamu toka Halmashauri za wilaya sita, Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufindi, Bahi na Kongwa. Wawakilishi toka masharika wanachama (INADES na UMADEP) pamoja na maafisa mradi wa PELUM Tanzania wakipewa maelezo na mmoja wa vijana waliopewa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa MAST.
 Timu ikichukua alama za shamba la mwananchi (wakiongozwa na mmiliki wa shamba) ili kuweza kupata mchoro kamili na ukubwa wa shamba husika.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...