*Aagiza viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wabadilike
*Ataka wasimamie wananchi waachane na matumizi ya mkaa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara, mashirika na taasisi zote za Serikali na binafsi zianze kutumia nishati mbadala ili kuondoa kabisa matumizi ya kuni na mkaa.
“Wizara, taasisi na mashirika yote ya Serikali na binafsi pamoja na vikundi vya uzalishaji wanaotumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia au shughuli za uzalishaji waanze kutumia nishati mbadala ili matumizi ya mkaa yaishe na ikiwezekana yatoweke kabisa,” amesema.
Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Mei 31, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Mkaa ni Gharama: Tumia Nishati Mbadala.”
Waziri Mkuu amesema teknolojia bora ya uzalishaji wa mkaa mbadala ambayo ameiona kwenye maonesho hayo, ikuzwe na kusambazwa kote nchini ili kuwawezesha wananchi walio wengi waachane na matumizi ya mkaa wa kawaida na badala yake watumie mkaa-mbadala kwa lengo la kuhifadhi misitu na kupunguza uharibifu wa mazingira.
Ili kufanikisha matumizi ya teknolojia hiyo, Waziri Mkuu amesema vibali vya ujenzi wa majengo makubwa na taasisi kama shule, vyuo, hospitali navyo pia vianze kuzingatia ufungaji wa mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya nishati mbadala katika taasisi na majengo makubwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa
uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari
kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua
Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam,
Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest
Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa
uliotengenezwa kutoka na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari
kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua
Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam,
Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest
Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Neema Matemba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa
mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo
wakati alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya
Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31,
2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Nimwagile Mwaijumba wakati
alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari cha Nyumbu na
kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka
iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea
mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January
Makamba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest
Ndikilo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David
Mwendapole wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia
gesi kidogo katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January
Makamba.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya
Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 30,
2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo,
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC
wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare
Matiku Makori na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, January Makamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...