Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi katika kituo cha Afya Chamwino. 

Jafo ameyasema hayo alipofanya ziara kituoni hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu unaofanyika katika kituo hicho.  

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo yanayojengwa na kwamba ni vyema ikaongezwa kasi ya ujenzi ili yakamilike kwa haraka. "Mafundi ongezeni kasi ya ujenzi kituo hichi cha Afya kikamilike haraka ili wananchi wapate huduma.  

Katika Zara hiyo, waziri Jafo pia amefanikiwa kufanya ukaguzi katika kituo cha Afya chamwino wilayani Chamwino pamoja na kituo cha Afya Mlali kilichopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma. 

Vituo hivyo viwili ni miongoni mwa vituo vya afya 208 vinavyoboreshwa na serikali ya awamu ya tano.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino  Athumani Masasi
 Jengo la upasuaji linalojemgwa katika kituo cha afya chamwino
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe.  Deo Ndejembi katika ukaguzi wa miundombinu ya kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa.
 Baadhi ya majengo mapya katika kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifurahishwa na uwekaji wa Tiles katika majengo mapya ya kituo cha afya Mlali Kongwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...