Na Mwandishi Wetu – Dodoma
Agizo alililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu la kuanzishwa kwa madawati ya kijinsia katika shule za Msingi na Sekondari nchini alilotoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike Novemba 2017 Mkoani Mara limeanza utekelezaji wake.
Utekelezwaji wa agizo hilo umeanza kwa kuanzishwa kwa Programu ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi wa shule za Sekondari katika kukabiliana na ukatili shuleni ambapo ndipo vitendo vingi vya ukatili ufanyika.
Programu hiyo iliyoanzishwa na Shirika la World Education na kuishirikisha Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye lengo la kuwajenga uwezo watendaji wanatekeleza afua za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto kuwa na mbinu za kuzuia, kuchukua hatua na kushughulikia wahanga wa ukatili shuleni.
Akifungua kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu hiyo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Marcel Katemba amesema kuwa Programu hiyo itasaidia kwa asilimia kubwa kuweka mazingira salama na rafiki kwa watoto kusoma bila kusumbuliwa na aina yoyote ya ukatili shuleni.
Ameongeza kuwa kupitia vitini vilivyopo katika Programu hiyo vitasaidia kuongeza weledi wa walimu kwa kubadili mitazamo na tabia zao na kuwa zenye nia ya kupinga vita ukatili na kuwa tayari kushughulikia vitendo vya ukatili punde vinapotokea.
Kaimu
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba
akifungua kikao baina ya Wizara na Shirika la World Education kujadili
Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari
kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Margareth Mussai akielezea jinsi
ukatili kwa watoto unavyoleta athari kubwa kwa watoto wakiwa wadogo na
wanapokuwa watu wazima katika kikao baina ya Wizara na Shirika la World
Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi wa
shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni kilichofanyika Jijini
Dodoma.
Mtaalamu
wa masuala ya Elimu kutoka Shirika la World Education, Grace Muro
akitoa taarifa ya hali ya ukatili kwa watoto ya mwaka 2011 ikionesha
kuwa msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 walifanyiwa ukatili wa
kingono kabla hawajafikisha miaka 18 katika kikao baina ya Wizara na
Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea uwezo waalimu
na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la World Education Tanzania, Lilian Badu akielezea
dhumuni la Shirika lake kutekeleza Programu ya kuwajengea uwezo waalimu
na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni katika
kikao kati ya Serikali na Shirika hilo kujadili Programu hiyo
kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mtaalamu
wa Masuala ya Kijinsia kutoka Shirika la Plan International Tanzania
Dkt. Katanta Simwanzi akielezea masuala mbalimbali ya ukatili wa
kijinsia na jinsi uanvyoleta madhara kwa jamii katika kikao baina ya
Wizara na Shirika la World Education kujadili Programu ya kuwajengea
uwezo waalimu na wanafunzi wa shule za Sekondari kupambana na ukatili
shuleni kilichofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi
ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto na Wadau kutoka Shirika la World Education wakijadilaina
kuhusu utekelzaji wa Programu ya kuwajengea uwezo waalimu na wanafunzi
wa shule za Sekondari kupambana na ukatili shuleni katika kikao
kilichofanyika Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...