Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa askari wake mmoja ameuawa na wengine watano hali zao si nzuri baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi kinachojulikana kwa jina la Siriri kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Taarifa ya kifo cha mwanajeshi huyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Ramadhan Dogoli ambapo akifafanua kuhusu kifo hicho amesema Juni kuwa 3 mwaka huu kikundi chetu cha wanajeshi , maofisa na askari ambao idadi yao ilikuwa 90 kikiwa katika uwajibakaji kilishambuliwa na kikundi hicho cha waasi.

Amefafanua sehemu ya kikosi hicho cha kulinda amani kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati(TANZBATT-1 CAR)baada ya kuanza kushambuliwa na waasi hao kwa kushtukizwa kiliamua kujibu mapigo.

"Kikundi chetu kilijihami kwa kujibu mapigo kijasiri na kufanikiwa kuwashinda nguvu washambuliaji na kwa bahati mbaya katika mapambano hayo askari wetu mmoja alipoteza maisa na wengine 18 walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao,"amesema.

Ameongeza kati ya hao waliojrehiwa askari watano hali zao si nzuri sana na kuongeza kuwa "askari wetu waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui katika Mji mkuu wa nchi hiyo".

Kanali Dogoli amesema mipango ya kuurejesha nyumbani mwili wa askari aliyepoteza maisha inafanywa na Umoja wa Mataifa na ikikamilika mwili huo utawasili nchini kwa taratibu za maziko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...