Baadhi ya wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni, Dodoma ambayo imeweka kipaumbele katika maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto), akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati), na Mhe. Janeth Masaburi baada ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 Bungeni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, wakiwa na furaha katika viwanja vya Bunge baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 kupita Bungeni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono wa pongeze na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kushoto), pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Bunge kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...