Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt.Salome Kassanga akitoa maelezo kuhusu wodi maalum ya viongozi wa Serikali iliyopo katika hospitali hiyo kwa wajumbe wa Kikosi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea Juni 25, 2018.
Baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma wakipata maelezo ya kuhusu hospitali ya Benjamini Mkapa kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa hospitali hiyo Dkt. walipotembelea Juni 25, 2018 Dodoma.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika dirisha la mapokezi hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Chuo kikuu cha Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Salome Kassanga akitoa maelezo kwa baadhi ya wajumbe wa Kikozi kazi cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma walipotembelea hospitali hiyo kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.
Kaimu Mkurugenzi Huduma za Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Salome Kassanga akitoa maelezo ya matumizi ya mitambo ya kuchunguza, kuzibua na Kutibu mishipa ya moyo iliyopo katika Hospitali hiyo walipotembelea kuona namna walivyojipanga katika utoaji wa huduma ya afya nchini.
Muonekano wa mashine za upasuaji wa matundu madogo (endoscopys) vilivyofungwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi.
Muonekano wa mashine ya CT-Scaniliyofungwa katika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...