Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
 ya mafundi ujenzi 800 wa jijini Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo maalum yakuwajengea uwezo wa kujua namna sahihi ya kufunga na kutumia vifaa vya kisasa vya ujenzi hasa vinavyotumika kutengeneza choo, bafu na kurembesha nyumba.
 Mafundi waliopata mafunzo wameongeza fursa za ajira pamoja na kuongeza kipato katika kuendesha maisha yao bila kuwa wategemezi. 
 Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Makurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Import International LTD , Trushal Jethwa wakati akizindua bidhaa mpya ya CERA ambayo utumika kutengeneza vifaa vya chooni, bafuni , mabeseni na urembo wa nyumba amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa na bidhaa bora . 
 Jathwa amesema kuwa waliamua kutoa mafunzo hayo baada ya kubaini uwepo wa mafundi wengi ambao hawana uelewa sahihi wa kufunga vifaa hivyo vya kisasa hasa vinavyozalishwa na CERA.
 "Licha ya kutoka mafunzo hayo pia tumekuwa tukiwaelimisha kutumia bidhaa zenye ubora hasa vya CERA ambayo imethibitishwa na viwango vya bora vya kidunia. Ni matumaini yangu kuwa bidhaa mpya tulizonunua leo zitachangamkiwa na watanzania wengi kwani gharama zake ni nafuu," amesema. 
Meneja Mauzo wa Kampuni ya International LTD , Hans Meleck ambao ndio wasambazaji wa bidhaa za CERA, Trushal Jethwa alisema ni muhimu kwa watanzania kutumia bidhaa zilizo bora hasa za CARE kwani upatikana kwa gharama nafuu ambayo kila mtanzania anauwezo wa kumudu. Meneja Mkuu Mwandamizi wa bidhaa za CERA ambazo uzalishwa nchini India, Dilip Thakker alisema bidhaa hizo zinauwezo kwa kudumu kwa zaidi ya miaka 12.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya International LTD, Trushal Jethwa akizungumza na waandishi wa habari wakati uzinduzi wa bidhaa mpya za CERA  kampuni hiyo kwa ajili ujenzi wa nyumba katika sehemu mbalimbali.
 Meneja Mkuu Mwandamizi wa Kampuni ya International LTD, Dilip Thakker akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampuni hiyo ilivyojipanga katika kuwafikia wateja kununua bidhaa CERA kama Gipsum, tiles na bomba kwa ajili ya ajili jiko, mabeseni.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Import International LTD ,Hans Meleck akizungmza na waandishi habari kuhusiana na bidhaa za CERA kuwa na ubora.
 Baadhi ya bidhaa za CERA zinazozalishwa  na kampuni ya ya International LTD

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...