Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

CHANGAMOTO ya ukosefu wa soko Katika Kijiji cha Manyovu Kata ya Munanila wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, imekuwa kero ya muda mrefu ambayo imesababisha wafanyabiashara wengi wa eneo hilo kukimbilia Kasulu na mikoa mingine.

Wanafanya hivyo kwa lengo kuendeleza biashara zao hali inayo sababisha kushuka kwa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

Wakizungumza na Michuzi Blog mkoani Kigoma mwananchi na mfanyabiashara wa Manyovu , Jackson Hemana amesema Soko litakapojengwa watapata faida kubwa na kwamba Warundi wamekuwa wakija Tanzania na kwenda kuchukua bidhaa katika Wilaya ya Kasulu kwa kuwa Manyovu hakuna soko.

Amesema litakapo jengwa wananchi wana muamko wa kufanya biasha na itasaidia pia hata kuongeza pato katika Wilaya na wananchi wote.Azalia Ashery amesema wao kama kafanya biashara wa mazao ya ndizi na nanasi pamoja na vyakula vingine wanapata shida na wanalazimika kuuzia biashara zao juani na mvua kuwanyeshea, hali inayosababisha mazao yao kuharibika na kupata hasara.

Pia amesema wafanya biashara wengine wanaamua kuuzia mazao yao shambani kutokana na ukosefu wa soko ambapo wanalazimika kuuza kwa bei ya chini kwani hakuna mahali watakapo kwenda kuuzia.

"Edapo Serikali itajenga jengo la soko itawasaidia sana wakulima kuinuka na kufanya biashara pamoja na kuinua Wilaya ya Buhigwe kwakuwa eneo hilo ni eneo maarufu kwa wakulima wa , Kahawa , Ndizi , Nanasi na Mazao mengine ya chakula na biashara hivyo yatapa soko na kuinua uchumi wa Watanzania," amesema.

Akizungumza ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia General Marko Gaguti amesema kutokana na changamoto hiyo wao kama viongozi wa Wilaya walishirikiana na kuandaa andiko la kuomba fedha serikalini kwaajili ya ujenzi wa soko la kimataifa litakalo wakutanisha wananchi wa Burundi na Tanzania kufanya biashara Katika soko la kimataifa ambalo litajengwa mpakani.

Amesema mradi huo umekubaliwa na hatua za awali zimekwisha kamilika ambapo Serikali kuu imetoa fedha Sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa soko lenye ghorofa moja litakalo kuwa na Ofisi 300 na maeneo ya vibanda vya wazi 500 na ujenzi utaanza mwaka wa fedha 2018/2019 na Julai mwaka huu watatangaza zabuni ya awali na ujenzi utatumia mwaka Mmoja.

"Sababu Kubwa ya kuuweka mradi huu Manyovu katika Wilaya ya Buhigwe eneo hilo ni eneo maarufu kwa Wilaya hiii na Mkoa kwa ujumla linalo wakutanisha Wafanya biashara Wengi kutoka Nchi za jirani kutokana na mpaka huo kutumiwa na Watu wengi ,soko hilo litakapo kamilika litatoa chagizo kubwa Kwa Wananchi wa Buhigwe na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kupata Fulsa ya Biashara na kuongeza pato katika Halmashauri ya Wilaya hiyo", alisema Brigedia Jenerali Gaguti.

Aidha aliwaomba Wananchi washiriki kwa pamoja katika ujenzi wa soko hilo pamoja na usimamizi ili malengo ya serikali ya kukamilisha mradi huo unao tarajiwa kuingizia kiasi cha shilingi milioni 230 kwa halmashauri hiyo ukamilike kwa wakati ilikuongeza ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.

Baraka Lupori ni Diwani wa Kata ya Munanila alisema anaishukuru sana Serikali kwa kuweza kuweka mradi mkubwa wa soko katika eneo hilo ambalo lilikuwa kilio kikubwa Kwa Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe na Kata hiyo ,ambapo Wafanya biashara wengi wa eneo hilo walikimbia kutokana na kukosa soko hali iliyopelekea kushuka kwa Mapato kupelekea kata hiyo kukusanya Kiasi cha shilingi milioni tatu tu kwa mwezi.

Alisema Munanila ni mpaka unaokutanisha Wananchi wa Nchi tatu za Burundi, Rwanda na Congo, na Wananchi wa Burundi wengi wa Burundi wanategemea sana Bidhaa za chakula kutoka Katika Vijiji vya Manyovu na Wilaya ya Buhigwe kwa ujumla soko hilo litakapo kamilika litasaidia sana wafanya biashara wengi walioondoka Manyovu na kuhamia maeneo Mengine kwaajili ya kuendeleza Biashara zao kurejea na kufanya biashara na kipato cha halmashauri na wananchi kitaongezeka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...