Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

WAZIRI wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jaffo ameishauri Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),kuhakikisha wanafungua matawi mengi zaidi Tanzania Bara.

Amesisitiza kufunguliwa kwa matawi hayo kutatoa fursa ya Watanzania wengi kuchukua mikopo fedha na hatimaye kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo hasa katika kipindi hiki cha ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Waziri Jaffo ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa shukrani zake kwa uongozi wa benki ya PBZ iliyokuwa imeandaa futari kwa ajili ya wateja wao, vingozi wa ngazi mbalimbali, watendaji wa benki hiyo na wananchi.

"Nitoe shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa PBZ kwa kuandaa futari hii ambayo kimsingi imetukunanisha watu wengi na wa kada tofauti.Nitumie nafasi hii kuwaomba muendelee kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli.

"Kwa sasa mmendelea kushuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikiendelea kufanyika nchini kwetu, hivyo ni vema mkaendelea kuuunga mkono juhudi za ujenzi wa viwanda unaotekelezwa."Uwepo wa benki hii ni muhimu kwani mchango wake ni mkubwa hasa pale inapotoa mikopo ya fedha kwa Watanzania wengi ambao nao kwa namna moja au nyingine wataweza kushiriki katika maendeleo ya nchi yetu,"amesema Waziri Jaffo.

Aidha amefafanua miradi ya ujenzi wa Reli ya kisasa(Standard Gauge), pamoja na mradi kuzalisha umeme katika Mto Rufiji (Stiggler’s Geogre) ni sehemu ya matokeo mazuri yanayoendelea kufanywa na Serikali ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Ameongeza tangu kuingia madarakani Serikali imepiga hatua kadhaa ili kuinua uchumi, ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na ununuzi wa ndege."Hii ni mikakati inayofanywa na Serikali yetu kuhakikisha inaboresha uchumi wake.Bila ya kuwa na uchumi imara itakuwa ngumu vijana kupata ajira."Hivyo ujenzi wa viwanda ni matokeo mazuri ya kufikia dhamira hiyo ambayo mbali na mambo mengine itawasaidia vijana wengi kupata ajira,"amesema.

Amesema kuna idadi kubwa ya wanaohitimu ngazi mbalimbali za masomo waliopo mitaani kutokana na kukosa ajira, hivyo ujio wa viwanda vya kutosha kwa kiasi kikubwa utasaidia vijana hao kutoka mitaani na kupata kazi.Kuhusu benki ya PBZ Waziri Jaffo amesema imejiapambanua vema kutokana na utoaji wa huduma bora na uwepo wa dirisha la Islamic ndani ya benki hiyo kumefungua milango kwa wale wanaotaka kukopa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam.

Hata hivyo wameshauri kujitanua mikoani kwa kufungua matawi maeneo mbalimbali nchini ili kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi nchini."Uwepo kwa dirisha la Islamic kumetoa fursa kwa waumini wa dini ya kiislamu kulitumia kupata huduma za kibenki.Kwa nafasi hii naombe muone fursa ya kuwasaidia vijana wengi kupata mikopo ya benki yenu ili kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi hasa uchumi wa viwanda,"amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Dirisha la Islamic la benki hiyo Said Mohammed Said akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa PBZ,amesema wanatoa shukrani kwa wateja wa benki hiyo kwa hatua zao za kuendelea kuunga mkono benki hiyo.

Amesema umefika wakati watanzania wachague huduma za benki hiyo ili waweze kunufahika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa kwa kutanguliza weledi wa hali ya juu katika kutoa huduma bora za kibenki."Tunatambua mchango wa wateja wetu katika kutuunga mkono na futari hii imetokana na wao kuwa pamoja nasi na ndio maana tumejumuika sote mahala hapa ,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...