Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba leo 28 Juni 2018 amefungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo, mkutano utakaotuama kwa siku mbili kuanzia leo mpaka kesho 29 Juni 2018 katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt Tizeba aliwasisitiza wajumbe wa baraza hilo kwa umoja wao kujadili kwa muktadha wa kutatua changamoto na kuboresha sekta ya kilimo kupitia mada mbalimbali zitakazowasilishwa ikiwa ni pamoja na kuhusu elimu ya majukumu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi, Elimu juu ya watumishi wa Umma na hoja kutoka vyama vya wafanyakazi sambamba na wajumbe kupitishwa katika bajeti ya wizara kwa mwaka 2018/2019.

Alisema kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu ambacho kimepewa nguvu kisheria ili kuwapa watumishi nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na ufanisi wa Taasisi ili kuongeza tija mahali pa kazi hivyo wajumbe hao wanapaswa kujadili mada hizo kwa ufanisi na tija.

Alisisitiza kuwa Baraza hilo linapaswa kuzaa matokeo mazuri ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya kazi huku akisema kuwa serikali imekuwa ikisisitiza kila taasisi ya umma kuunda mabaraza ya wafanyakazi ili kuongeza ufanisi na tija katika mchango wa mapinduzi ya uchumi wa viwanda.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Katibu wa Baraza la wafanyakazi Wizara ya kilimo Bi Agnes Hugo wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa mkutano na uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...