Na Shani Amanzi, 

Mkuu wa Wilaya wa Chemba Mhe.Saimon Odunga amewataka Watendaji na Wataalam wa Halmashauri kusimamia Sheria ndogo za katika ngazi za kata na vijiji katika kuendelea kuisimamia ili kuthibiti uharibifu wa mazingira.

Mhe.Saimon Odunga amesema “ikiwa leo ni siku ya Mazingira Duniani na utaratibu huu hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe moja mpaka sita ,mwezi Juni hufanyika maadhimisho haya, kwa hiyo ni lazima kuzuia viashiria hivyo ikiwemo ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na kuni,uchomaji moto ovyo misitu,utupaji takataka ovyo,kilimo katika maeneo ya miteremko mikali na uchimbaji wa mawe”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Halmashauri ya Chemba kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wanaendelea na Kampeni ya kupanda miti ndani ya Wilaya ya Chemba.

“Kwa mwaka huu wa 2018-2019 tunatarajia kupanda miti laki tano ,hii ni utekelezaji wa mpango ulioasisiwa na Makam wa Rai,Mhe Samiah Suluhu wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani sambamba na kuisaidia jamii kupata nishati ya kupikia kama vile kuni”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara wa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Chemba ,Mohamed Semdoe amesema kwa kushirikiana na Viongozi katika ngazi za Kata na Vijiji ,tunaendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Pia Idara ya Usafi na Mazingira imeanzisha mkakati wa kutenga maeneo ya dampo katika ngazi za vijiji pamoja na kuhamasisha jamii zishiriki katika kuchangia gharama za uzoaji taka kutoka katika maeneo ya makazi na biashara.

Kauli mbiu ya mwaka huu Kitaifa ni “MKAA NI GHARAMA;TUMIA NISHATI MBADALA” ambapo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa dampo la Kijiji cha Kidoka ,Kata ya Kidoka, Tarafa ya Goima wilayani Chemba,tarehe 5/6/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba,Saimon Odunga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa dampo la Kidoka,katika kijiji cha kidoka wilayani Chemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...