Na Agness Francis,Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wametia saini na wizara ya afya kutekeleza mpango wa kuzuia magonjwa ya kuambukizwa kupitia viwanja vya ndege. Mpango huo ni endelevu ulioanzishwa na shirika la ndege la kimataifa la usafiri wa anga duniani.

Ambapo kama wanachama wa shirika hilo ambao ni wadhibiti wa mamlaka ya afya nchini wanajukumu la kuchukua mpango huo na kuuandaa kwa kushirikiana na wizara ya afya pamoja na wadau mbalimbali wizara nyingine mbalimbali.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari amesema kuwa dhumuni ni kuhakikisha uboreshaji ili kujihakikishia Tanzania inapambana na magonjwa ya maambukizi yanayotokana na usafiri huo wa anga kwa njia ya muingiliano wa watu kutoka sehemu mbalimbali,  ukizingatia nchi jirani ya Jamuhuri Kidemokrasia ya Congo mlipuko wa ungojwa wa ebola umeshaua watu takribani 15.

Johari amesema pia ni utaratibu huo utawezesha watumiaji wa usafiri wa anga kusafiri kwa usalama.

Mkuu wa vituo vya afya wiwanja vya ndege, bandari na mipaka Remidius Kakulu amesema kuwa mpango huo ukianza utekelezaji wake itasaidia kupambana na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama ebola.

"Katika viwanja  vyetu vyote vya ndege tumefunga vipimo vya kupima joto ambapo abiria  wote wanaoingia nchini watapimwa,kwa atakaeonekena na joto kali atawekwa pembeni kwa ajili ya uchunguzi zaidi"amesema Kakulu.

Aidha kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara mamlaka ya  usafiri wa anga Tanzania Daniel Malanga amesema kuwa usafiri huo ambao wa haraka kuliko yote ndio unaoweza kusambaza magongwa kwa kasi zaidi kwa kutumia mpango huo muhimu kwa kushirikiana na wadau wengi wa viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchin utasaidia kuzuia maambukizi hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari akitia saini leo ikiwa ni makubaliano ya kutekeleza mpango wa kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuambukizwa kupitia viwanja vya ndege hapa nchini katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza Johari(katikati) pamoja na Kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa kiuchumi na biashara wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Daniel Malanga kushoto mara baada ya zoezi la utiaji sani kumalizika leo Jijini Dar ea Salaam.
Picha ya pamoja wadau mbali mbali mara baada ya zoezi la uwekaji wa saini kumalizika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...