VIJIJI 1O vya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ikiwemo cha Kongowe wamepatiwa elimu ya afya na vizazi rika pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali kuhusu magonjwa yasiyo ambukiza.

Elimu na mafunzo hayo yametolewa na Shirika la HelpAge Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya Jb Geriatric pamoja na HIV Center.

Mkurugenzi wa Asasi ya Jb Geriatric Judith Bagachwa amesema elimu na mafunzo hayo yametokana kupitia nguvu ya kijiji katika tekelezaji.Amesema lengo ni kuwawezesha wanakijiji kutumia rasilimali walizo nazo pasipo kutegemea kupata msaada wowote ule kutoka vyanzo vya nje.  

"Mradi huu ulichaguliwa na wanakijiji wenyewe wa Kongowe ambao kwa busara zao waliona ni kitu ambacho kingeweza kunufaisha wanakijiji wote,"amesema. Pia ameongeza kwa muda mrefu toka mradi huo uanze Kongowe imekuwa ikisuasua hasa katika utekelezeji. 

"Wanakijiji walikubaliana kuanzisha shamba la bustani ya kulima mbogamboga ili kuwasaidia wazee na pia watu mbalimbali kupata lishe bora,"amema.Pia wanakijiji walikubaliana kutoa elimu ya dawa ya kulevya ili kuwasaidia vijana ambao walionekana kuathirika na janga hilo. 

 Akieleza kwa undani kuhusu jitihada zilizofanyika Mzee Gadi Salumu Matitu amesema haikuwa rahisi kwani kila mtu alitegemea wangewezeshwa katika kuufanya  mradi huu. "Wengi walisahau kuwa ilitupasa kutumia rasilimali tulizonazo ili kufanikisha mradi huu,"amesema. 

Mmoja wa walioshiriki  kutekeleza mradi huo Shaha Iddi amesema rasilimali waliyokuwa nayo ilikuwa nguvu tosha ya kufanikisha mradi wa kijiji ila watu wengi wamekuwa wakitaka kuwezeshwa kwanza ili kuweza kufanya kitu.Naye Mariam Ally anasema penye nia pana njia. Hiyo imejidhihirisha sasa kwani pamoja na changamoto zilizopo wamefanikiwa kufanikisha lengo lao.

Mshiriki mwingine katika mradi huu wa Kongowe Salma Hamadi Salum amesema mradi huo umekuwa wa manufaa kwao kama washiriki na hata pia jamii. 
Mahindi kutoka shamba lo kongowe baada ya kuvunwa na sasa yanapikwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja ambao ni wana kongowe. 

Baadhi ya washiriki wa Mradi wa kijiji Kongowe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...