Takribani
wateja 500,000 wanatembelea Jumia ndani ya mwezi katika mwaka huu 2018,
kutoka wastani wa wateja 250,000 kwa mwezi mwaka 2017.Makampuni ya Kiafrika zaidi ya 60,000 na wafanyabiashara wamejiunga na Jumia.
Ikiwa
na dhamira ya kutengeneza mustakabali wa mazingira mazuri ya masoko na
fursa za kuuza na kununua bidhaa pamoja na huduma za mtandaoni na
kifedha, Jumia inaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya huduma za manunuzi ya mtandaoni barani Afrika.
Ikiwa
imeanzishwa mwaka 2012, Jumia inajivunia kufanya kazi na makampuni
zaidi ya 60,000 ya Afrika pamoja na wafanyabiashara wa kiafrika kwenye
mtandao wake.
Akizungumzia
juu ya shamrashamra za maadhimisho haya yakatakayodumu kuanzia Julai 2
mpaka Julai 15 mwaka 2018, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok
Prescott amebainisha kuwa sherehe za mwaka huu zimekuja sambamba na
sikukuu za Sabasaba hivyo kutoa fursa zaidi kwa wateja kununua bidhaa
mbalimbali kwa gharama nafuu na ofa lukuki.
“Sabasaba
ni maonyesho makubwa ya kibiashara siyo tu nchini Tanzania bali kwenye
ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Ni muhimu kwa wafanyabiashara
na wateja ambapo hupata fursa ya kufanya maonyesho ya bidhaa na huduma
tofauti, kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Kwa maneno mengine, Jumia
ni kama maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kwa njiaya mtandao.
Siku
zote Jumia ina aina tofauti za bidhaa zinazopatikana kwa bei nafuu
kabisa. Kwa hiyo sherehe za Jumia kwa mwaka huu itashiriki maonyesho ya
Sabasaba, na kuwapatia wateja (watakaokuwepo Sabasaba na maeneo mengine)
fursa ya kununua bidhaa kwa punguzo kubwa la bei, kujishindia zawadi,
vocha za manunuzi na ofa kemkem kutoka mtandaoni na washirika wetu,”
alisema Bw. Prescott.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia barani Afrika na uzinduzi wa kampeni ya Sabasaba. Kulia ni wawakilishi kutoka kampuni ya simu ya FERO, ambao ni mojawapo ya washirika wa Jumia katika maonyesho ya Sabasaba mwaka 2018.
Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionesha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba katika banda la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini katikati ni muwakilishi mwenza kutoka FERO Javid Bapu huku kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...