KAMPUNI ya simu ya Infinix kuzindua simu mpya ikiwa ni muendelezo wa Infinix NOTE 4 kwa kushirikiana na GOOGLE. Uzinduzi huo unategemewa
kufanyika mnamo mwezi wa sita barani Afrika nchini Dubai katika jengo la Burj Khalifa.

Kwa pamoja ikishirikiana na GOOGLE kampuni ya simu ya Infinix imeweka nia ya kuzindua simu
iliyo na ubora zaidi ya matarajio ya wengi na inasemekana kupitia ushirika wake na GOOGLE ujio wa simu zote za NOTE kutumia mfumo wa Android 1 (A1) wenye ufanisi zaidi ya Android
Oreo.

Zaidi ya watu 200 mpaka sasa wameshapata mwaliko kutoka katika kampuni hizo mbili kwendakushuhudia uzinduzi huo pamoja na kushuhudia namna Android 1 (A1) inavyofanya kazi kupitia
GOOGLE Assistant na GOOGLE Lens.

Akiongelea mafanikio ya kampuni, muongeaji wa kampuni ya Infinix Bwana Erick Mkomoyealisema kwamba, “tangu kutambulishwa kwa kampuni ya Infinix mwaka 2013, kampuniimeweza kudhihirisha ubora wake na kuweza kupenya katika masoko ya Afrika na tuko mbionikuwaletea teknolojia mpya kupitia simu mpya itakayozinduliwa wiki ijayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...