*Kamishna wa Bima nchini atoa ufafanuzi , aipongeza kampuni ya Sanlam kwa kutimiza miaka 100


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMISHNA wa Bima nchini Dk.Baghayo Saqware amesema kuanzia Agosti mwaka huu kampuni za bima nchini yataanza kusajili mawakala wa bima wao wenyewe kadri wanavyoweza huku mchakato wa ununuzi wa bima kwa njia ya kibenki ukiendelea.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kutimiza miaka ya 100 ya kampuni ya bima ya Sanlam tangu kuanzishwa kwake.Hivyo mbali ya kuipongeza Sanlam kwa kutimiza miaka 100 akatumia nafasi hiyo kutoa majibu ya changamoto ambazo ziliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sanlam Ibrahim Kduma.

Kaduma pamoja na kuzungumzia mafanikio ya kampuni hiyo kwenye masuala ya bima ametaja changamoto tatu ambazo zinakwamisha sekta ya bima nchini.Changamoto hizo ni masharti magumu ya kusajili wakala wa bima, kuchelewa kwa mchakato wa benki kutumika kununua bima pamoja na kodi kubwa.

Hivyo Dk.Saqware amewahakikisha watoa huduma za bima nchini kuwa tayari yameandaliwa mabadiliko ya sheria na hivyo kampuni ya bima itakuwa na uwezo wa kusajili mawakala wengi kadri ya uwezo wao.

Kuhusu benki kufanya shughuli za bima Dk.Saqware amefafanua changamoto hiyo nayo itapata ufumbuzi hivi karibuni kwani hivi sasa wanaandaa kanuni na Agosti mwaka huu watazipeleka kwa wadau ili wazipitie na kisha kuanza kutumika bada ya kupata baraza za Waziri.

"Kuhusu benki kufanya shughuli za bima hili lilichekelewa kwasababu Benki Kuu Tanzania(BoT) ilikuwa inataka kujiridhisha na sas imekubali , hivyo ni changamoto ambayo kimsingi imepata ufumbuzi wake na kilichobaki ni kuandaliwa kwa kanuni ili benki nazo zitumike kwenye masuala haya ya bima"amesema.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance, Khamis Suleiman (wapili kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya kampuni hiyo.Hafla hiyo iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Ibrahim Kaduma (kulia) pamoja na viongozi wengine akigonganisha glasi pamoja na wateja wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya Sanlam tangu kuanzishwa kwake. Wa tatu kushoto ni Kamishna wa Bima Dk Baghoyo Sakwale ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pia wadau mbalimbali wa masuala ya bima walihudhuria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...