Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa  mtandao wa Jamii Forums, Micke William baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu.

Max na Micke wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi  Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona kuwa ushahidi uĺiotolewa na mashahidi hao dhidi ya washtakiwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha na kuongeza kuwa hauna mashiko. 

Katika kesi hiyo namba 457 ya mwaka 2017 washtakiwa wanatuhumiwa kuwazuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi.

Kabla ya uamuzi huuo kutolewa leo, awali washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali  Mutalemwa Kishenyi ambae alidai  Melo na William  ni wamiliki na waanzilishi wa mtandao wa Jamii  Media Co Ltd ambao umesajiliwa Brela Julai 2 mwaka 2008 na kupewa namba ya usajili 66333 

Alidai baada ya usajili, hupatiwa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo wa kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Aidha katika maelezo hayo, Kishenyi  alidai Mei 10 mwaka 2016, ZCO aliwaandika barua washtakiwa akiwafahamisha ofisi yake inafanya upelelezi kuhusu taarifa ya uongo dhidi ya Cusna Investment na Ocean Link iliyochapishwa na  mwanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri. ZCO pia aliwafahamisha  kwa kifupi taarifa ambayo anaihitaji kutoka kwao  na maelezo binafsi ya mtu aliyechapisha  ili aweze kufanya upelelezi.

Alibainisha kuwa Mei 11mwaka  2016 mfanyakazi wa Jamii Media, Chrispin Mganyizi aliipokea na kuiwasilisha kwa washtakiwa  lakini walikwamisha polisi kufanya upelelezi kwa kuficha taarifa za wanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri.

Kishenyi alidai kuwa kufuatia jitihada hizo za ZCO za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...