Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAFANYAKAZI wanne wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wenzao wawili wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia TPA hasara ya Sh.26,041,782.73,ambapo Juni 18 mwaka huu watasomewa maelezo ya awali (PH).
Washtakiwa ambao watasomewa PH katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba ni Masoud Suleiman Kova (36) mhasibu wa TPA washtakiwa wengine ni Lydia Kimaro (52) mhasibu TPA, Ally Mkango (54) Oparesheni ofisa wa TPA na Aron Luisinga (35) mhasibu TPA. Wengine ni wafanyakazi wa benki ya CRDB, Grace Komba (41) na Juma Ng'oka (41).
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini bado hajamaliza kuiandaa.Hivyo taarifa hiyo, kesi imeahirishwa hadi Juni 18 mwaka huu.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kushindwa kuzuia kutendeka kwa kosa na kusababisha hasara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...