WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikali kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema watakaobainika kuhujumu mifumo hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia watumishi wasio waadilifu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 23, 2018) mara baada ya kuzindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU) ni  “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu”. 

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini, wananchi, Sekta Binafsi, Sekta ya Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa na Wadau mbalimbali,  kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.

“Hii ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa  ambayo yamehimizwa na Kaulimbiu ya mwaka huu,”.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kwenye uzinduzi wa mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Shukran George kwa niaba ya mwanae Magreth Msomba, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga, wakati akikagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...