MKUU  wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe amelitaka Shirika la  Bima la Taifa  (NIC) kuongeza maarifa na ubunifu wa kutafuta masoko mapya  kutokana na kuwepo zama za ushindani mkubwa wa kibiashara.
Dk Kebwe alisema  hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliofanyika mjini Morogoro.
Alisema , pamoja na kuongeza masoko mapya pia ni vyema shirika likajizatiti katika ulipaji wa madeni kwa wateja wao ,kwa kufanya hivyo kutadumisha imani kwa wateja na kuongeza biashara kwa kiasi kikubwa.
Mkuu mkoa alisema, baraza la wafanyakazi  ni chombo muhimu katika ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kufikia maamuzi mbalimbali na katika kuongeza tija
Pamoja na hayo alipongeza Shirika hilo kwa kukuamua kuanzisha bima ya kilimo kwa wakulima na hatua hiyo itauwezesha  mkoa wa Morogoro ambao ni  moja wenye fursa kubwa ya kilimo  kunufaika zaidi.
“ Ningependa kuwaomba bima hii ya kilimo itakapoanza mkoa wangu  upewe nafasi ya kupata elimu hii, wakulima wengi wa mkoa wa Morogoro waweze kunufaika nayo” alisema Dk Kebwe.
Pia alilipongeza kwa hatua mbalimbali za kidigitali walizofikia ikiwem matumizi  ya Tehama na mfumo wa kidigitali wa Comesa ambao wanatarajia kuanza kuutumia.
Mkuu huyo wa mkoa pia alilitaka Shirika hilo kutumia vyema rasilimali watu walizonazo na teknlojia hiyo ili kufikia malengo yaliyowekwa ya biashara .
Kwa upande wake  Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Sam Kamanga   kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Morogoro, kufungua mkutano  huo alisema , mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu isemayo “ Bima ya Kilimo ni Udondo Rutuba kwenye Kilimo Biashara na Uchumi wa Viwanda Imara”.
Kamanga  alisema , katika mkutano huo wa siku mbili  kulikuwa na mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo pamoja na mafunzo ya mfumo mpya wa kidigitali wa Comesa
 Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la  Bima la Taifa  (NIC), Sam Kamanga  ( kulia) akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kushoto),kwa ajili ya kufungua mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC.
  Wajumbe wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC wa kimsiliza mgeni rasmi
  Wajumbe wa mkutano wa nane wa baraza la wafanyakazi wa NIC wa kimsiliza mgeni rasmi

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kati kati mwenye koti walioketi ) akiwa na baadhi ya viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) chini ya Mkurugenzi mtendaji hilo,  Sam Kamanga  ( watatu  kutoka kushoto walioketi) 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( kati kati mwenye koti walioketi ) akiwa na viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) chini ya Mkurugenzi mtendaji hilo,  Sam Kamanga  ( watatu  kutoka kushoto walioketi) mara baada ya mkuu wa mkoa kufungua mkutano wa nane wa baraza hilo.( Picha na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...