Na Munir Shemweta, Liwale 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesuluhisha mgogoro ulipo katika kijiji cha Kichonda kilichopo wilayani Liwale mkoa wa Lindi baina na wakazi wa kijiji hicho kuhusu uhawishaji wa ardhi ya kijiji ekari 1000 kwenda kwa muwekezaji M/S KSM & AGL EXPORT FARM C LTD. 
Wananchi wa kijiji cha Kichonda wamekataa uhawishaji wa ardhi ya kijiji hicho kwenda kwa muwekezaji kwa madai kuwa muwekezaji huyo ameshindwa kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa kwa wakazi hao kabla ya kumilikishwa rasmi eneo hilo. 
Kwa mujibu wa wakazi wa kijiji hicho, muwekezaji huyo aliwaahidi wakazi hao kuwajengea msikiti, kuwachimbia kisima cha maji, kusaidia magodoro katika zahanati ya kijiji lakini wamedai kuwa kutotekelezwa kwa ahadi zote hizo kumewafanya kukosa imani naye na kueleza kuwa hastahili kumulikishwa eneo hilo. 
Hata hivyo, baadhi ya wananchi walieza kuwa, muwekezaji huyo kwa sasa hapaswi kulaumiwa kwa kuwa eneo lenyewe hajapewa jambo linalomuwia vigumu kwake kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa hivyo walitaka akubaliwe kumilikishwa ndipo waanze kumlaumu.
 Naibu Waziri Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Lindi kuhusiana na masuala ya Ardhi alipowasili mkoani humo jana kwa ziara ya siku mbili.
e
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa halamshauri ya Manispaa ya Lindi, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemaga na kushoto ni mbunge wa Viti Maalum Hamida Abdallah (Picha na Munir Shemweta- WANMM).
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kichonda wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi  wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji hicho kwa muwekezaji.
.
 Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kichonda akichangia maoni wakati naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi alipotembelea kijiji hicho kuhakiki zoezi la uhaishwaji ekari 1000 kwa muwekezaji.
.

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kichonda wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (hayupo pichani) wakati wa kuhakiki uhaishwaji wa eneo la ekari 1000 za kijiji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...