Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Westham ya Uingereza Wilfried Bony akiwa na watoto wenye mahitaji maalumu huko Kigamboni jijini Dar es salaam alipowatembelea Jumatatu na kuwapa misaada mbalimbali. Bony, ambaye amewahi kuchezea pia Swansea na Manchester City, yupo nchini kwa ziara binafsi na anatarajiwa kuondoka baadaye leo. Kwa mujibu wa msemaji wake, Bony ataongea na vyombo vya habari saa tano na nusu hoteli ya Protea Oysterbay jirani na kanisa la mtakatifu Peter.
Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast na Westham ya Uingereza Wilfried Bony akiwa kwenye pantoni ya MV Magogoni akivuka kutoka kwenye kambi ya watoto wenye mahitaji maalumu huko Kigamboni jijini Dar es salaam alipowatembelea na kuwapa misaada mbalimbali.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...