Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imesema katika kukuza biashara nchini imesema inatarajia kuzindua Muongozo wa Uendeshaji Viwanda nchini Julai 2, mwaka huu kupitia Serikali Mitaa ili kutekeleza lengo la ufufuaji na uendeshaji viwanda nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya Maonyesho ya 42 Sabasaba, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Ole Gabriel, amesema tayari Serikali imeridhia uanzishwaji wa mchakato huo.

Alisema tayari mikakati mbalimbali inaandaliwa kuhakikisha mkakati huo unakua endelevu. Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda na ili kufikia malengo tutazindua mpango huu,"alisema Gabriel.

Profesa  Ole Gabriel sema kauli mbiu ya Maonyesho ya Sabasaba mwaka huu ni ukuzaji Biashara kwa ajili ya maendeleo ya Viwanda. Gabriel alisema, kauli mbiu hiyo imeteuliwa kwa lengo kukuza uchumi wa viwanda hapa nchini.

Amesema unapoangalia uchumi wa viwanda ni lazima uangalie bidhaa zinazouzwa ndani ya nchi," alisema Gabriel. Alisema Serikali ya awamu ya Tano imejidhatiti kuweka uchumi wa viwanda hivyo ni wajibu kwa kila taasisi itengeneze bidhaa bora itakayoingia katika uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (Tantrade), Edwin Rutageruka, alisema wanakuza biashara ili kupata kodi, ajira na kukuza viwanda nchini.

Amesema maonyesho ya mwaka huu, yatafunguliwa Julai 2, ambapo hadi hivi sasa tayari wageni 33 wametoka nje ya nchi na  washiriki wa ndani ni 2,956  na taasisi za Serikali 127.

"Tunashukuru kwa mwaka huu washiriki wa nje wameongezeka kwa mwaka jana walikuwepo 30,"alisema Rutageruka
Katibu  Mkuu  Wizara ya Viwanda na Uwekezaji  Profesa Olisante Ole Gabriel, akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa  Shirika  Simu  Tanzania (TTCL) Rachael Mremi kuhusu huduma ya  4G wakati alipotembelea banda la shirika hilo, katika Maonyesho ya 42 ya  ya  Kimataifa ya Biashara, viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, B, Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...